https://monetag.com/?ref_id=TTIb Sita waua kwa kupigwa risasi Mtwara | Muungwana BLOG

Sita waua kwa kupigwa risasi Mtwara


Watu sita wameuawa katika kijiji cha Ngongo Wilaya ya Tandahimba mkoani  Mtwara na wengine saba kujeruhiwa katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana.

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz amesema Watanzania sita walipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kutoka nchi jirani ya Msumbiji wakati wakiwa visiwa vya mto Ruvuma wanakofanya shughuli za kilimo.

“Usiku walivamiwa na kikundi cha watu waliowakusanya pamoja na kuwapiga risasi. Watu sita walifariki dunia na wengine saba walijeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Tandahimba.”

“Jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola tutachukua hatua madhubuti kuhakikisha wote waliohusika na tukio hili wanapatikana na kuchukuliwa hatua,” amesema DCI Boaz.

Aidha wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhali wanapokwenda nchi nyingine kufanya shughuli za kiuchumi.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberatus Sabas amesema kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ndio maana wahalifu wanafanya matukio hayo mipakani.