TAKUKURU yaagizwa kumshikilia na kumchunguza kiongozi wa Kijiji


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani humo kufanya uchunguzi kumbaini mfugaji alietumia mhuri wa serikali ya kijiji na kuandika barua ya malalamiko kudai kuna hali ya uvunjifu wa amani katika kijiji cha kambala na kuipeleka Ofisi ya Rais Tamisemi.

Agizo hilo la Mkuu wa Mkoa linakuja akiwa katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Kambala Wilaya ya Mvomero Mkoani hapa kikao kilicho lenga kutekeleza agizo la waziri wa  TAMISEMI  la kumtaka Mkuu wa Mkoa kufika kijijini hapo  kusikiliza hoja za wakazi hao.

Ambapo wakazi hao wengi wao ni jamii ya wafugaji kilicho mshangaza Mkuu wa Mkoa pamoja na wajumbe wake wa kamati ya ulinzi na usalama, wenyeviti  hao kukataa kuhusika na suala hilo la kuandika barua.

Hali hiyo inamlazimu Mkuu wa Mkoa kuitaka TAKUKURU kuingilia kati suala hili kuchunguza nani alie husika kuandika barua hiyo, akianza na viongozi walio tajwa moja kwa moja.

Barua iliyo andikwa septemba 27 mwaka huu wa 2019 imeeleza imetoka kwa wananchi wa kijiji hiki cha kambala kwa uwakilishi wa mwenyekiti wao wa serikali ya kijiji, kwenda ofisi ya rais tamisemi ikimtaka kushughulikia hali ya uvunjifu wa amani katika kijiji chao