Waziri Mkuu Majaliwa kuzindua mkakati mpya wa Kitaifa wa kidijitali jijini Dodoma

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mkakati mpya wa kitaifa wa Afya wa kidijitali utakaofanyika Novemba 14 mwaka huu jijini Dodoma.

Mkakati huo wenye lengo la kufanya maboresho kwenye sekta ya Afya umeandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais-TAMISEM ambapo unatarajiwa kuifanya Tanzania kuwa mojawapo ya wa Nchi viongozi ulimwenguni katika afya ya kidijitali.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Tiba Wizara ya Afya ,Maendeleo ya jamii,jinsia na Watoto,Dk Grace Magembe amesema kuwa mojawapo ya mambo muhimu kwenye mkakati huo ni muundo wa utawala ambao unaongeza meno na ufanisi katika mkakati tekelezaji wa mkakati huo.

” Viungo viwili vikuu vitawajibika kimsingi katika mkakati huu navyo ni Kamati ya usimamizi wa afya ya kidijitali na Sekretarieti ya Afya ya Kidijitaki Kitaifa,” Amesema Dk Grace.

Dk.Magembe amesema kuwa  mkakati huu mpya wa kitaifa ni wa miaka mitano hadi 2024 na utaenda sambamba na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2024, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya (2015-2020) na sera zingine muhimu zinazohimiza juhudi Nchi kujenga mifumo madhubuti ya kidijitali inayoweza kuwasiliana na sekta ya afya.

Aidha Dk.Magembe amesema kuwa Serikali inatarajia kuzindua maktaba ya kidijitali kuhakikisha kuwa kuna uwazi na wadau wanapata taarifa juu ya mipango iliyopo ya afya na hati zote.

” Pamoja na uzinduzi huo unaotarajia kufanyika wiki hii tayari kuna kazi zinaendelea kufanyika katika uwanja wa Jamhuri wananchi wameendelea kujitokeza kwa kupima afya zao bila malipo yoyote hivyo tunaomba waendelee kujitokeza kwa wingi ili kupima afya zao”

Aidha Dk.Magembe amesema pia watazindua mpango wa magonjwa yasiyoambukiza ambapo moja ya Kazi ya mkakati huu wa kidijitali ambao utazinduliwa utakuwa unahifadhi  takwimu za magonjwa yasiyoambukiza, ili  kufuatilia rasilimali zote zinazoingia kwenye huo mpango je zinaleta tija? Lakini pia tuwe na taarifa muhimu za haya magonjwa je zinaongezeka au zinapungua.

Dk.Magembe amesema kuwa wao kama Wizara wameamua kwenda na mpango huo wa kidijitali ili kuwa na Benki ya takwimu lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa sekta ya afya nchini.

Mpango huo unatajwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 100 na umeandaliwa kwa muda wa miezi sita hadi kukamilika.

Dk Grace amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza kupima afya zao sambamba na kufanya mazoezi ambayo yamekua muarobaini wa magonjwa yasiyoambukiza.

” Sekta ya afya ni sekta ambayo inabadilika sana, kila siku magonjwa mapya na tiba mpya zinakuja, mpango huu utakua msaada kwenu tutakapohitaji kufanya tafiti maana tutakua na takwimu ya kile tunachohitaji kukifanyia utafiti.

Hata hivyo amesema kuwa mfumo huu wa kidigitali utasaidia kuangalia zile takwimu zetu na tutazifatilia ili kuona kama kuna mabo mapya yanatokea ni kwanini kwa hiyo tutatumia takwimu zetu ili kufanya utafiti,mpango huu wa kidigitali unaenda kuwa mkombozi kwenye sekta hii muhimu ya Afya.