https://monetag.com/?ref_id=TTIb Aliyefungwa miaka 30 na kutoka kwa msamaha wa Rais mke ampa zawadi watoto wanne | Muungwana BLOG

Aliyefungwa miaka 30 na kutoka kwa msamaha wa Rais mke ampa zawadi watoto wanne



Na James Timber, Mwanza

Mkazi wa Tabora anayetambulika kwa jina la Timotheo Silasi miongoni mwa wafungwa walioachiliwa kwa msamaha wa Rais Dk. John Magufuli akiwa na umri wa miaka 20 alikuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani Butimba jijini Mwanza, kwa kosa la unyang'anyi, afurahishwa na  mkewe wa ndoa kumletea nyumbani watoto wanne.

Akiongea na Muungwana Blog, Mhanga huyo wa kifungo amempongeza mama mkwe wake kwa kumfundisha maadili mema mke wake, kwani toka aanze kutumikia adhabu hiyo mkewe alihamia karibu na gereza hilo kutoka mkoani Tabora ili awe anamuona kumhudumia mumewe.

Bw. Silas aliongeza kuwa katika kutumikia adhabu hiyo kwenye Gereza la Butimba alibahatika kupata taaluma mbalimbali ikiwemo ufundi mwashi na  mafunzo ya biblia katika ngazi ya cheti ambapo ujuzi huo ulichangia kutoka mara kwa mara nje ya gereza na kuwaiona familia yake pale apitapo barabarani na gari la magereza.

Bi.Magdalena ambaye ni mke wa Bw. Silasi amesema kuwa alichukua maamuzi ya kuhamia jijini Mwanza na kwenda kupanga karibu na gereza hilo kwa lengo la kumhudumia mumewe kwa mahitaji madogo kama sabuni na mafuta ya kujipakaa huku akiwa anafanya biashara za kuuza mboga na matunda ili kulisha familia.

Hata hivyo pamoja na kuachiliwa kwa msamaha wa Rais Bw. Silasi amesema kuwa makosa aliyokutwa na nayo hayakuwa na ukweli kwani alipakaziwa na wanakijiji baada ya kupigwa sana na jeshi la sungusungu na mama yake mzazi kutishiwa maisha aliamua kukiri kosa kuwa alikuwa mnyang'anyi na kutaja watu ambao alishirikiana nao kwa kubashiri majina ya uongo.

Aidha ameiomba jamii impokee kwa mara nyingine atakaporudi kijijini kwani kwa sasa ni mwinjilisti wa kanisa la Seventh Day Adventist Wasabato, pia amewasamehe wale wote walioshiriki kumpakazia kesi na kumuomba mkewe waishi kwa amani ili wafikie malengo waliojiwekea siku ile waliofunga ndoa.