Loading...

12/02/2019

Kaka wa mfalme wa Saudia afariki akiwa na umri wa miaka 88

Ndugu wa kambo wa Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia, Prince Muteb bin Abdulaziz, amefariki akiwa na umri wa miaka 88.

Kulingana na kituo cha habari cha Saudia SPA,sababu ya kifo cha Muteb haikutolewa na marehemu atazikwa baada ya kusaliwa katika msikiti mtakatifu wa Makkah.

Ujumbe wa rambirambi uliotolewa na Mahakama ya kifalme ya Saudi Arabia umesema kwamba Muteb bin Abdulaziz alikuwa mmoja wa wana wa Mfalme Abdulaziz, mwanzilishi wa Ufalme wa Saudia.

Bin Abdulaziz, ambaye pia alikuwa mshiriki wa Ujumbe wa Biat, alimteua Mfalme na Mwanamfalme wa nchi hiyo na kufanya kazi katika baadhi ya wizara mpaka mwaka 2009.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger