Korea Kaskazini yafanya majaribio ya kombora

Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kufanya majaribio mengine ya kombora kwenye satellite yake, haya yakiwa ni maendeleo ya hivi karibuni ya nchi hiyo.

Shirika la habari la Korea kaskazini KCNA limeripoti kwamba serikali ya Korea Kaskazini imesema hatua hiyo ni kwa ajili ya kujilinda na kitisho cha mashambulio ya nyuklia kutoka Marekani.

Majaribio hayo yalifanyika siku ya Ijumaa katika kituo cha Sohae cha kufanyia uzinduzi wa satellite.

 Mkuu wa itifaki Pak Jong Chon ameonya kwamba maadui wa Korea Kaskazini pamoja na Marekani wanapaswa kujiepusha na kuikasirisha Korea Kaskazini iwapo wanataka kuiona amani katika mwaka mpya.