Loading...

12/05/2019

Lowassa atoa neno Sumaye kuhama CHADEMA


Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa amesema hawezi kusema chochote kuhusu ya hatua alizozichukua Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, kutangaza kukihama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Lowassa ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na EATV Digital ambayo ilimtafuta ikitaka kujua mtazamo wake kutokakana mwaka 2015 wote wawili walihamia chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

"Kuhusiana na suala hilo kwa sasa mimi siwezi kuzungumza chochote nadhani ungeniacha tu" amesema Lowassa ambaye tayari amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Ikumbukwe Jana Disemba 4, 2018, wakati akitangaza uamuzi wa kuhama chama hicho, Sumaye alidai sababu kubwa ya kuhama ni kukosekana kwa Demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho.


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger