https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mmiliki wa Clouds aeleza sababu nyimbo za Diamond kutochezwa | Muungwana BLOG

Mmiliki wa Clouds aeleza sababu nyimbo za Diamond kutochezwa


Mmiliki wa Kampuni ya Clouds Media, Joseph Kusaga ameeleza sababu ya nyimbo za msanii nchini humo Diamond kutopigwa wala kuchezwa katika kituo cha redio Clouds na Clouds Tv.

Kusaga ameyasema hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha Bartender ambapo kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na kwa nini kituo hicho hakipigi nyimbo za Diamond.

"Tulipiga ngoma ya Mbosso siku moja, tukaulizwa kwa nini hatujapiga kwa miaka mitano nyimbo za Diamond na kutakiwa kuandika barua ya kujieleza."

"Mimi Kusaga niandike barua mimi Kusaga niandika barua ya kupiga, kwani napata hasara gani kama ni biashara zangu zinaendelea tu si umetaka nifunguke?." Kusaga alimuuliza mtangazaji huku wakicheka.

Hata hivyo Kusaga ametaka sakata hilo kuulizwa Menejimenti ya wasafi huku akisema meneja wa Diamond, Tale na Salaam hana tatizo nao kwani ametoka nao mbali.