Loading...

12/02/2019

Mvua yasababisha vifo nchini India

Watu 17 wamepoteza maisha wakiwemo watoto wawili na wanawamke wanne baada ya ukuta wa nyumba kuanguka katika jimbo la Tamil Nadu nchini India.

Kulingana na ripoti za wanahabari wa India, ukuta wa mita 16 umeangukia nyumba tatu kutokana na mvua kubwa kunyesha katika kijiji kilicho karibu na mkoa wa Coimbatore.

Maafisa walisema nyumba hizo zilianguka na watu 17 walipoteza maisha.

Mamlaka imeripoti kuwa tukio hilo limetokea asubuhi na mapema, wakati wenye nyumba walipokua bado wamelala.

Kwa upande mwingine, idadi ya vifo na ajali zilizosababishwa na mvua kubwa tangu mwisho wa wiki imeongezeka hadi kufikia watu 22.

Uongozi wa Tamil Nadu,umetangaza kwamba jamaa za wale waliopoteza maisha watalipwa rupe elfu 400 (karibu pauni elfu 32) kama fidia.

Mitihani imeahirishwa katika vyuo vikuu kadhaa kutokana na mvua kunyesha katika mkoa huo.

Masomo yamesitishwa katika baadhi ya maeneo huko Tamil Nadu baada ya kutangazwa kwa mvua kubwa kwa muda wa siku mbili.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger