Loading...

12/12/2019

Rais Magufuli atoa neno kwa wajumbe NEC kuhusu uchaguzi wa serikali za Mitaa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amewapongeza Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kwa kuweza kushinda uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Rais Magufuli ambaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ametoa kauli hiyo wakati anafungua Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Inayofanyika Jijini Mwanza .

"Nilianza kwa kuwapongeza kwa kushinda uchaguzi wa serikali za Mitaa na kuwakumbusha kuhusu mageuzi tuliyoyafanya kwenye Chama chetu na mafanikio yaliyopatikana kutokana na mageuzi hayo na mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wangu" alisema Rais Magufuli

Aliendelea kwa kusema, "Ninyi wajumbe wa NEC ndio vyombo muhimu wa kuleta mabadiliko katika Taifa hili, hayupo mwingine wa kuwasemea na hata patikana kwa sababu serikali hii inaongozwa na Chama cha Mapinduzi".
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger