https://monetag.com/?ref_id=TTIb RC Kagera awapa kazi Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya | Muungwana BLOG

RC Kagera awapa kazi Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya


Na. Clavery Christian, Bukoba Kagera

Mkuu wa mkoa Kagera, Brig. Jen. Marco E Gaguti amewaagiza wakurugenzi na wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha wanatenga fedha za huduma ya chakula kwa watoto wadogo kulingana na watoto walioko kwenye halmashauri ikiwa ni lengo la kupambana na udumavu wa akili kwa watoto unaonekaka kuwa mwingi mkoani licha ya mkoa huo kuwa kati ya mikoa mitano bora hapa nchini inayozalisha chakula kingi.


RC Gaguti amesema kuwa eneo la kwanza ambalo mkoa huo halifanyi vizuri ni eneo la utoaji fedha kwenye mipango ya halmashauri ambapo amesema kuwa taarifa aliyoipokea mara ya mwisho halmashauri zote zilikuwa na alama nyekundu ikiashiria hatari kwa sababu ya kushindwa kutenga fedha na kuzitoao ambapo kila halmashauri inapaswa kutenga shilingi elfu moja kwa kila mtoto.

"Moja wapo ya jambo la kwanza ambalo nataka tuliwekee mikakati na maazimio baada ya kikao hiki ni kuhakikisha halmashauri zetu zote tunatenga fedha kulingana na idadi ya watoto tuliyonao ili kuhakikisha tunawanusuru watanzania hawa, inawezekana leo tukaona maumivu ya fedha kwasabu ya mipango tuliyonayo au changamoto ya bajeti lakini faida zake ni kubwa mara miamoja zaidi sababu unafanya ukombozi wa kijana mwenyewe" Amesema RC Gaguti.

Amesema kuwa lengo la kuhimizwa kutoa shilingi elfu moja kwa kila mtoto mdogo chini ya miaka mitatu ni kiweza kumkomboa huyu mtoto ili serikali isiendelee kumuhudumia maisha yake yote kwasababu ikishindwa kumuhudumia hapa ni kwamba itaweza kumuhudumia maisha yake yote kitu ambacho itakuwa ni hasra kwa serikali. Nakiwata viongozi wa idara mbalimbali kutochukulia swala la lishe kama swala la kawaida.

"Naomba tusichukulie swala hili kirahisi mtu anasema mboma hafi yawezekana alisha kufa kama ubongo wake upo chini ya asilimia 50% ni bahati ya Mungu tu mti huyu anakuwa amekufa" Amesema RC Gaguti.

Kwa upande wake Afisa Lishe kutoka TAMISEMI, Bi Bertha Mwakabage amesema kuwa changamoto kubwa sana ni kupambana na udumavu kuanzia kwenye unyonyeshaji ndo maana wanataka mtoto apatiwe vyakula vyenye kuleta virutubisho kwa kutengeneza ubongo mzuri wa mtoto kwa kunyonya na kula vyakula vinavyomjenga mtoto akiwa bado mdogo.