https://monetag.com/?ref_id=TTIb Uchafuzi wa hali ya hewa wasababisha shule kufungwa Iran | Muungwana BLOG

Uchafuzi wa hali ya hewa wasababisha shule kufungwa Iran

Uchafuzi wa hali ya hewa umepelekea kufungwa kwa shule za msingi na zile za  sekondari katika mji mkuu wa Tehran, nchini Iran.

Wagonjwa wa moyo na mapafu na wanawake wazee na wajawazito huko Tehran watapatiwa likizo na nauli katika usafiri itapunguzwa.

Gavana wa Tehran Enushirevan Muhsini Bendpey amesema kuwa kulingana na kituo cha upimaji wa ubora wa hewa ya jiji, uchafuzi wa hewa katika mji mkuu umedhamiriwa kukithiri na hii inaweza kusababisha shida za kiafya kwa wagonjwa wenye mzio.

Bendpey hapo awali amethibitisha kuwa gharama za usafirishaji wa umma zitapunguzwa.

Mbali na yote magari ya zamani na mamilioni ya pikipiki ni moja ya sababu zinazoongeza uchafuzi wa hewa huko Tehran. Tehran imechukua safu ya 12 katika orodha ya uchafuzi wa hewa ulimwenguni.