Ufaransa: Upepo, mafuriko vyasababisha umeme kukatika na watu kukosa makazi

Mamia ya watu walilazimika kuyaacha makazi yao, kutokana na upepo mkali na mafuriko nchini Ufaransa.

Upepo huo na mafuriko vilivyoangusha miti na kusababisha kukatika kwa umeme vimesababisha kifo cha mtu mmoja.

Watu wengine watano walijeruhiwa baada ya miti kuangukia magari yao siku ya Ijumaa. Mamlaka nchini humo zinafanya kazi kurejesha umeme katika maelfu ya makazi ya watu.

Maji ya mafuriko hayo yaliripotiwa kuongezeka kwa futi moja kila baada ya saa moja hapo jana katika baadhi ya maeneo.

Kampuni ya kutoa huduma ya Enedis imesema, hadi kufikia Jumamosi jioni takriban kaya 25,000 zilikuwa bado hazijarejeshewa huduma ya umeme.