Umuhimu wa kusema samahani katika mahusiano ya mapenzi



Wanapokuwa watu wawili kwenye mahusiano, lengo lao linakuwa ni moja ambalo ni kupendana. Lakini kuna misunderstanding ambayo huwa hahikosi kwa wawili hawa hata kama ni wakamilifu kiasi gani. Cause no one who is perfect always!! Ila kuna jambo ambalo huwa lipo katikati yao pia ambalo ni kuelewana, na safari inaendelea.

Kwenye mapenzi kuna njia tofauti ambazo zinaweza kuonekana kutatua migogoro inayojitokeza ikiwa ni pamoja na kutumia washauri, lakini kuna dawa moja kubwa sana katika mahusiano na mapenzi kama to say am sorry, samahani ni neno dogo sana lakini matokeo yake ni makubwa sana.

Kusema samahani haimaanishi wewe ni mjinga, au hauna akili au wewe ndio ni mwenye makosa.

Samahani inapunguza mabishano na maneno mengi, inarudisha maelewano ndani ya nyumba.

Inahitaji moyo husiobeba visasi, ina maana kutopiliza kisasi kwa lililotokea hapo awali.

Lakini kwa kuliongelea swala hili ni rahisi sana lakini kwa kulitenda ni vigumu sana, fikiria kama wewe ndio umemkosea mpenzi wako alafu pale pale wewe ndio uombe msamaha,

unafikiri hilo ni rahisi kufanyika? Na vipi kama wewe umekosa na ukaomba msamaha husisamehewe utafanya nini? Will u walk out?? Na ni mara ngapi umetumia neno samahani kwa siku? Na je mahusiano yanaweza kudumu bila samahani??

Bila shaka hakuna mahusiano yanayoweza kudumu bila kujua thamani iliyopoa katika neno samahani, hivyo kusema samahani ni muhimu sana katika mahusiano ili kulifanya penzi lenu liwe bora zaidi.