https://monetag.com/?ref_id=TTIb Urusi na China wazindua mradi wa bomba la gesi | Muungwana BLOG

Urusi na China wazindua mradi wa bomba la gesi

Urusi na China leo zimezindua bomba kubwa la gesi linalounganisha nchi hizo mbili kwa mara ya kwanza, ikiwa ni moja ya miradi mikubwa mitatu inayolenga kuifanya Urusi kuwa muuzaji mkubwa wa gesi duniani.

Rais Vladmir Putin wa Urusi na rais Xi Jinping wa China wamesifu bomba hilo la gesi kama alama ya ushirikiano.

Hafla hiyo iliyoonyeshwa kupitia televisheni na kuwaunganisha kwa njia ya vidio, imewaonyesha wafanyakazi na njia ngumu ya bomba la gesi kutoka mashariki mwa Siberia hadi kwenye mpaka na China.

Bomba hilo la gesi lenye urefu wa kilometa 3,000 ambalo Putin ameliita mradi wa ujenzi mkubwa duniani, utaisambazia China kiasi cha bilioni 38 za gesi katika kipimo cha ujazo kwa mwaka pindi utakapoanza kufanya kazi mwaka 2025.

Urusi na China zilitia saini ujenzi wa mradi huo utakaogharimu dola bilioni 400 mwaka 2014.