Viongozi wa serikali za mitaa wilayani Nachingwea watakiwa kuhudumia wananchi bila ubaguzi



Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Viongozi wa vijiji na vitongoji waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa wilayani Nachingwea, wametakiwa kuhudumia wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa.

Agizo hilo limetolewa leo katika kata ya Kilimanihewa, wilaya ya Nachingwea, na mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Hamisi Chitanda wakati wa hafla ya kuwapongeza viongozi hao.

Chitanda alisema  viongozi waliochaguliwa hawanabudi kuwahudumia wananchi wote bila kujali itikadi ya vyama vyao vya siasa. Kwani wao ni viongozi wa serikali.


Alisema japokuwa viongozi hao wametokana na CCM, lakini hiyo ilikuwa ni tiketi tu ya kuwa viongozi wa serikali ambayo lengo lake ni kuwahudumia wananchi wote.

Chitanda alisema serikali itaendelea kuwapelekea maendeleo wananchi kama ilivyokawaida yake. Kwani inatambua vema kwamba maendeleo hayana chama.

 '' Niwaombe wananchi wawaunge mkono viongozi wetu katika shughuli maendeleo. Kmani sio ya chama cha siasa, bali ya wananchi wote,'' aliseme Chitanda. Mjumbe huyo wa kamati ya siasa  alisema viongozi hao watende haki. Kwani CCM imejengwa kwa misingi ya haki.

Aliwaonya viongozi hao wasijione ni mabosi wa wananchi, bali watumishi wao. Wakiwamo wanyonge.

'' Mmeaminiwa na chama, kwahiyo utumishi wenu nzuri utajenga msingi wa ushindi katika uchaguzi mkuu ujao,'' Chitanda  alisisitiza.

 Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka huu, wagombea waliopitia CCM kwa wanafasi zote za uongozi wa serikali za mitaa katika wilaya ya Nachingwea wamepita bila kupingwa.