Baba mbaroni kwa tuhuma ya kutoka kimapenzi na mwanae wa darasa la 5

Na Amiri kilagalila-Njombe

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe linamshikilia mkazi mmoja  wa  mtaa  wa  Joshoni Halmashauri ya Mji Njombe , Hezron  Ndone  (44)  kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wake mwenye umri wa miaka 11,ambayo yalikuwa yakilalamikiwa  na mke wake kwa mda mrefu mpaka wananchi walipopaza sauti juu ya tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issa   amethibitisha  kukamatwa  kwa  mtuhumiwa  huyo, Hezron Ndone ambaye ni mfanyabiashara wa mkaa na kusema pindi taratibu zitakapokamilika atafikishwa mahakamani.

“Katika hali isiyokuwa ya kawaida baba huyu ametumia mbinu zake chafu kumuamisha mkewe kwenye chumba chake na kumpeleka chumba kingine na akaamua kumchukua mwanae na kukaa naye kwenye chumba chake,na matokeo yake imetokea madhara, na baba huyu tunamshilia kwa kuwa na mahusiano kati yake na mtoto wake ambayo yalikuwa yanalalamikiwa na mama mtu kila mara mpaka wananchi wamepaza sauti na jeshi lilienda kuhakikisha jambo hili limekuwa ni mgogoro katika familia”alisema kamanda Hamisi Issa