Bajaji zaidi ya 25 zakamatwa kwa kukiuka sheria za usalama barabarani

BAADA ya mgomo wa daladala uliotokea hivi karibuni mkoani
Iringa jeshi la polisi limeendesha oparesheni kali na kuwakamata madereva
bajaji zaidi ya 25 kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.

Akizungumza na blog hii, Kamanda wa kikosi cha usalama
barabarani mkoani Iringa, Yusuph Kamotta alisema kuwa zoezi hilo la kuwakamata
madereva bajaji wanaokiuka sheria za usalama barabarani limetokana na migomo midogo
ya madereva daladala inayotokea kutokana na mgongano wa kimaslahi hali
inasababishwa na madereva bajaji kuingia katika barabara wasizoruhusiwa.

Alisema kuwa zoezi hilo linafanywa na jeshi la polisi baada
ya changamoto kubwa kutokea katika barabara kuu ya Iringa kuelekea Dodoma
ambapo kwa kiasi kikubwa inasababishwa na mwingiliano ambao bajaji wanatumia na
kuleta mgongano dhidi ya daladala kutokana na kugombea abiria hali ambayo
inajitokeza mara kwa mara.

Kamotta alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu na
kuwataka madereva wote wa bajaji na daladala kufata sheria ambazo wamekuwa
wakitoa mara kwa mara madereva hili kuondokana na hali ya migomo ya mara kwa
mara inayoweza kutokea kwa sababu ya mwingiliano.

“Ndugu mwanabahari tumekuwa tunatoa mara kwa mara elimu kwa
madereva wote sisi kama sisi lakini pia kupitia viongozi wao lakini kuna baadhi
ya madereva ambao wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani na hao ndio
chanzo kikubwa hivyo zoezi hili limefanyika na kuwakamata zaidi ya 25 ambao
lazima wafikishwe mahakamani” alisema

Alisema kuwa kutokana na kukiuka sheria za usalama
barabarani kwa madereva hao jeshi la polisi linawashikilia na wanapelekwa
mahakamani na kuwataka kufata sheria bila shurti kwani jeshi la polisi kitengo
cha usalama barabarani kiko imara na zoezi litafanyika kila siku hadi kuondoa
migomo isiyokuwa ya lazima inayosababishwa na wachache.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa  Waendesha Daladala mkoa wa Iringa, Ambakisye
Mwangomba alisema kuwa wamekuwa wakikabiliana na changamoto ya bajaji kufanya
kazi ambazo kama daladala wakati biashara yao inatakiwa kukodiwa na zaidi
wamekuwa na kondokta kama wapiga debe.

Alisema kuwa baada ya madereva kugoma hivi karibu tulikaa
meza moja na kamanda wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani na
kuangalia changamoto hizo za bajaji zinatatuliwa vipi kitu ambacho kimefanyiwa
kazi na kuona bajaji zinazokiuka sheria zikichukuliwa hatua na kufanya hali ya
usafiri kuwa salama.

“Leo tumeona jitihada za mkuu wa kikosi cha usalama
barabarani namna ambavyo anafanya kazi na hali ya usafiri imekuwa shwari kwani
wale bajaji wanaokiuka sheria wanakamatwa wao na vyombo vyao na natoa wito kwa
jeshi kuendelea kufanya oparesheni ili kuwabaini wanaokiuka sheria hizo”
alisema

Alisema kuna baadhi ya madereva wa bajaji wanavunja sheria
kwa makusudi licha ya elimu wanayopewa na hii inaweza kuwa ni udogo wa adhabu
wanazopewa hivyo kuna umuhimu wa kuongezewa adhabu na kufikishwa mahakamani
kuweza kuondoa kabisa wavunja sheria.

Alisema kuwa changamoto kubwa iko katika suala la bajaji
kupitia njia ambazo daladala zinapita hasa kwenye njia kuu ambazo wao
hawaruhusiwi kupita na kufanya biashara kama ambavyo daladala wanafanya hali
ambayo inasababisha madereva daladala wasifanye biashara na kuwapa wakati mgumu
kufikisha kiwango walichopangiwa na wamiliki wa daladala.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa waendesha Bajaji manispaa ya
Iringa, Melabu Kihwele alisema kuwa operasheni inayoendelea inatokana na
madereva bajaji kupita katika barabara ambazo hawaruhusiwi hivyo kuvunja makubaliano
yaliyowekwa walipoketi pamoja, bajaji daladala, Sumatra, mkuu wa wilaya na
jeshi la usalama barabarani na kufikia mwafaka wa daladala wananjia na zao na
bajaji wananjia zao.
“Madereva bajaji wam
ekuwa wanakiuka sheria kwa makusudi
kutokana na tayari walishapewa elimu mara kwa mara na hata sisi viongozi
tumekuwa tukiendelea kuwaelimisha kuhusu kufata sheria za barabarani lakini
bado wamekuwa wakikiuka sheria hizo na hali inayopelekea jeshi la polisi kikosi
cha usalama barabarani kuwakamata na kuwafikisha mahakamani”alisema.