IGP Sirro aungana na watanzania kuadhimisha miaka 56 ya mapinduzi zanzibar

Jeshi la polisi limewataka watanzania wote katika kuadhimisha miaka 56 ya mapinduzi kudumisha amani, utulivu, usalama na mshikamano.

Akitoa ujumbe huo Inspekta jenerali wa polisi, (IGP) Simon Nyakoro Sirro amesema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana kuzuia na kupambana na uhalifu wa aina zote.

''Ninaungana na Watanzania wote katika kuadhimisha miaka 56 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar tuendelee kudumisha amani, utulivu, usalama, umoja na mshikamano wetu" amesema IGP Sirro.