Jeshi la Sudan lazima jaribio la uasi

Jeshi la Sudan linayashikilia makao makuu ya kikosi cha usalama wa taifa cha nchi hiyo ambacho awali kilikuwa kitiifu kwa rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir, ripoti zinaeleza.

Mapambano yalianza Jumanne katika jiji la Khartoum ambapo milio ya milipuko ilisikika.

Kitengo hicho cha usalama wa taofa kwa sasa kinavunjwa.

Serikali inaadai kuwa uasi huo umechochewa na mlipo ya mafao, lakini pia kuna mashaka juu ya tukio hilo kulenga kuchelewesha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Kiongozi mwandamizi wa baraza huru linaloongoza Sudan kwa sasa, Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, amemtuhumu mkuu wa zamani wa usalama wa taifa Salah Gosh kuwa yupo nyuma ya uasi huo.

Japo Dagalo anasema hachukulii jambo hilo kama jaribio la mapinduzi, lakini amesema jambo hilo halivumiliki.

Kumekuwa na wasiwasi juu ya uwezekao wa baadhi ya viongozi waliokuwa na ushawishi wakati wa Bashir kujaribu kutatiza mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo kwa hivi sasa.

Bashir ambaye alikaa madarakani kwa mkono wa chuma kwa miaka 30 alipinduliwa mwezi Aprili mwaka jana baada ya kuchacha kwa maandamano ya umma.

Askari kutoka kitengo cha usalama wa taifa walipakia mtandaoni picha za video zikionesha wenzao wakifyatua risasi hewani usiku kama alama ya uasi na kuonesha nguvu zao.

Shirika la habari la Reuters linanukuu raia wakidai kuwa kulikuwa na mapambano ya katika wilaya ya kaskazini Khartoum, na jengo la usalama karibu na uwanja wa ndege kutekwa na waasi.

Vyanzo ndani ya jeshi vinaeleza kuwa vikosi vya serikali kwa sasa vimerejesha hali ya utulivu katika maeneo ambayo waasi walikuwa wakishambulia baada ya kufanya mazungumzo nao.

Kundi kubwa la waandamanaji wa nchi hiyo wametoa wito wa kukomeshwa kwa "oparesheni hizi zisokuwa na msingi ambazo zinawatia hofu wananchi."