Loading...

1/16/2020

Mke wa Mabeste afunguka A-Z kilichomkimbiza kwenye ndoa yake

Mwanzilishi wa harakati za Piga Kambi Utalii wa Ndani, Lisa Karl Fickernscher ambaye alikuwa ni mke wa msanii wa Hip Pop hapa nchini Mabeste amefunguka kiundani kuhusu maisha yake na aliyekuwa mume wake.

Maisha ya wawili hao yalikuwa maarufu zaidi kupitia mtandao wa instagram ambapo watu wengi zaidi pasi kujua nyuma ya pazia ya maisha yao walikuwa wakifurahia familia yao na kutamani kuwa kama wao.

Ambapo Lisa kupitia Youtube chaneli ya simulizi na sauti amefunguka mazito ukweli kuhusu maisha ya mahusiano yao nje ya kile ambacho mashabiki wengi walikuwa wanakiona kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Ndoa si siri tena, juzi tumeyasikia ya Stamina kupitia sanaa yake leo Lisa amefunguka kinagaubaga sababu ambazo zimepelekea kuvunja ndoa yake na Mabeste na yapita mwaka sasa tangu wawili hao kufarakana.

Akihojiwa Lisa amehadithia sababu kuu mbili za kuachana na Mabeste ambapo ametaja kuwa Mabeste alikuwa mwanaume mwenye mkono mwepesi wa kumpiga hata mbele ya watoto wake , lakini pia ameeleza kuwa Mabeste hakuwa mwanaume wa kujitoa na mtafutaji kwaajili ya familia yake.

Pili amesema kwa asilimia 80 Mabeste alikuwa hasimamii majukumu yake kama baba wa familia na mume kwake.

”Hakuwahi kusimamia majukumu yake, sikuwahi kula hela ya muziki wake,… Kuna tofauti kubwa sana kati ya mkulima anayeenda shambani analima lakini hapati mavuno kuliko yule ambaye hafanyi kitu anashonda tu nyumbani… Mabeste alikuwa mzito sana infika stage mnagombana nageuka kama mzazi kwake namlea kama navyolea watoto” amesema Lisa

Lisa ameongezea ”Alikuwa hataki kufanya chochote, kunipenda sio kusema unanipenda kunipenda ni matendo, sikuajiliwa, mwenzangu alirelax hakuwa na wivu mwanamke nimehudumia familia miezi miwili mitatu, alikuwa hata hajiulizi natoa wapi hakuwa na wivu”.

Aidha Mabeste na Lisa wameachana yapita mwaka sasa wakiwa na watoto wawili, Kendrick na Catelyn Mabeste.

Pia tumeona kumekuwa na mfumuko wa matukio ya aina hiyo ya ndoa za watu maarufu kufarakana jambo ambalo si jema sana kwani linatishia pakubwa sana wale wanaotarajia kuingia kwenye ndoa.

Tumeona Stamina na mke ndoa yao ikiwa na doa na Stamina kupitia sanaa yake ameamua kuweka wazi kisa mkasa.

Ndoa ni fumbo zito sana, ni Mungu tuu azijalie ndoa amani, upendo na ushirikiano kwani kila ndoa ina changamoto yake ni namna tu mnavyoweza kutatua changamoto hizo ili kusogeza familia.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger