Mkuu wa mkoa wa Kagera awaapisha wajumbe wa baraza la ardhi


Katika kuendelea kutatua migogoro ya Ardhi hapa Nchini, Mkuu wa Mkoa Kagera amewaapisha Wajumbe wawili wa mabaraza ya ardhi kutoka Wilaya za Missenyi na Bukoba ili waweze kuendelea kutoa katika masuala yahusuyo katika maeneo yao.

Wajumbe hao walioapishwa Januari 20, 2020 ni Pamoja na Bi. Mary Kokuleba Mtaajwa na Bi. Jinesta Banyenza Rugakingira, katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera, ikihudhuriwa na wadau wa sheria, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini, Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kanda ya Bukoba, Jaji Lucia Kalio, pamoja na Jaji wa Mahakama Kuu  Kanda ya Bukoba Jaji Angela Anthony Bahati.

Wakitoa nasaha zao kwa nyakati tofauti Mara baada ya kuapishwa Kwa wajumbe hao, Viongozi hao wamewataka Wajumbe hao kusimamia na kutenda haki katika masuala yote yahusuyo ardhi hasa kutatua migogoro isiyo ya lazima, hii ni kutokana na ardhi kuendelea kuwa na Thamani kubwa katika maisha ya kila siku, na ni vyema kuendelea kuheshimu taratibu na sheria za ardhi zinvyoelekeza.