https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mwanaume akichepuka kwenye ndoa inakuwa maarufu kuliko mwanamke- Nikki wa Pili | Muungwana BLOG

Mwanaume akichepuka kwenye ndoa inakuwa maarufu kuliko mwanamke- Nikki wa Pili

Mwanamuziki wa HipHop kutokea kampuni ya Weusi Nikki wa Pili, amesema kwenye mahusiano ya ndoa, Baba akichepuka ndiyo inakuwa maarufu zaidi kuliko Mama anapochepuka.

Nikki wa Pili amesema mara nyingi mwanaume anapokuwa kwenye mahusiano au ndoa ambayo hataki kutoka ni ngumu kumwambia mtu matatizo yake.

"Mwanaume kama yupo kwenye mahusiano au ndoa ambayo na hataki kutoka ni ngumu sana kumwambia mtu kosa kama hilo, hawezi kusema kama amechepuka nje ya ndoa au mke wake kamsaliti, kwa sababu kijamii heshima ya mwanaume  katika tendo kama hilo likivunjika ni ngumu sana kuirudisha, lakini kwa mwanamke ni tofauti" ameeleza Nikki wa Pili.

Nikki wa Pili ameendelea kusema "Ikigundulika kama mama fulani mwanaume wake amemsaliti, jamii inaweza isione kitu kibaya sana, kwa mwanaume kama mke wake ndiyo anafanya vitendo hivyo inakuwa ni nzito, na mara chache sana kumkuta baba anawaeleza watoto makosa ya mama, lakini utakuta mama hueleza makosa ya baba" ameongeza.