Mzee Samatta afunguka mwanae kuelekea kutua Uingereza

Baba wa nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta anajivunia mafanikio ya mtoto wake katika ulimwengu wa kandanda.

Mzee Ally Pazi Samatta ameielza BBC kuwa imekuwa ni ndoto yao yeye na Mbwana siku moja kuona mshambuliaji huyo akitua Uingereza na kusakata kabumbu.

Ndoto hiyo inakaribia kukamilika wakati huu ambapo Aston Villa inatumai kukamilisha makubaliano ya dau la £10m kumsajili mshambuliaji huyo wa klabu ya Genk ya Ubelgiji.