https://monetag.com/?ref_id=TTIb Ndege ya Iran yaanguka barabarani baada ya rubani kukosa mwelekeo | Muungwana BLOG

Ndege ya Iran yaanguka barabarani baada ya rubani kukosa mwelekeo

Ndege ya abiria ya Iran ilijipata katika barabara ya umma baada ya kuteleza katika barabara ya uwanja wa ndege ilipokuwa ikitua.

Hakuna hata mmoja kati ya abiria wote 135 walioabiri ndege hiyo aliyejeruhiwa katika mkasa huo uliotokea kusini magharabi mwa mji wa Mahshahr.

Ndege hiyo ya kampuni ya Caspian iliondoka mjini Tehran . Matairi yake hayakujitokeza kabisa wakati ilipotarajiwa kutua.

Picha za abiria waliokuwa wakitoka katika ndege hiyo zilichapishwa katika mitandao ya kijamii.

Runinga ya serikali ilinukuu maafisa wa usafiri wa angani wakisema kwamba rubani aliishusha ndege hiyo kuchelewa hivyobasi akakosa barabara ya ndege.

Ripota mmoja ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo alisema kwamba matairi ya nyuma ya ndege hiyo yaliharibika na kwamba ndege hiyo iliteleza bila matairi yake.

Msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani Reza Jafarzadeh aliambia chombo cha habari cha Isna news kwamba ndege hiyo iliteleza kutoka katika barabara yake siku ya Jumatatu alfajiri .


Iran ina rekodi mbaya ya safari za ndege . Watu 66 walifariki katika ajali ya ndege mnamo mwezi Februari 2019, huku makumi wakifariki 2019 wakati ndege ya IranAir ilipovunjika vipandevipande baada ya kuanguka 2011.

Muungano wa Ulaya umepiga marufuku kampuni mbili za ndege kutotumia anga yake kutokana na wasiwasi wa kiusalama.

Iran ilikuwa imepanga kuimarisha ndege zake zilizozeeka baada ya vikwazo vya miaka mingi kuondolewa ikiwa ni miongono mwa makubaliano ya mkataba wa kinyuklia wa 2015 na mataifa yenye uwezo mkubwa.

Hatahivyo wizara ya fedha nchini Marekani ilifutilia mbali leseni ya kampuni kuuzia Iran ndege za abiria baada ya rais Donald Trump kujiondoa katika makubaliano hayo 2018.