VIDEO: Rais Magufuli amteua mrithi wa Lugola, Zungu aula


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo amemteuwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.


Simbachawene anachukua nafasi ya Kangi Lugola, ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo Januari 23, 2020 na Rais Magufuli kwa kile alichoeleza kutoridhishwa na utendaji kazi katika Wizara hiyo.

Pia Mhe. Rais Magufuli amemteua Mussa Azzan Zungu kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na George Simbachawene aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi.


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE