VIDEO: Waziri Ndalicha ''Hatukuwa matapeli kwa wananchi'


Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia, Profesa Joyce Ndalichako pamoja na balozi wa China hapa nchini,WANG  Ke leo wameshiriki uwekaji wa jiwe la msingi la sekondari ya mfano ya masomo ya Sayansi mkoani Arusha iliyopewa jina la mkuu wa mkoa huo MRISHO GAMBO.

Shule hiyo ya kisasa ambayo kwa mkoa wa Arusha ni ya kwanza itakayokuwa ikiendeshwa kwa mfumo wa kisayansi (STEM) yaani SAYANSI,TEKNOLOGIA,UHANDISI,NA HISABATI,Ipo katika kata ya Olasity jijini ambayo hadi sasa tayari  madarasa manane ya kisasa yamekamilika na tayari wanafunzi wamenza kuyatumia pia ina maabara nne za kisasa, chumba cha  Kompyuta,nyumba za walimu na madawati ambapo madarasa mengine na jengo la utawala bado vikiendelea kujengwa.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE