Yafahamu mambo ambayo mwanamke anayahitaji katika mahusiano ya kimapenzi

1. Anataka mume anayemjali na kujali kila anachokitaka. Sio tu mahitaji ya kimwili, bali pia ayatambue mahitaji yake ya kisaikolojia, upendo na kujali hisia zake.

2. Anataka mume anayemlinda na kumfanya ahisi kuwa yuko salama wakati wowote, kiasi kwamba hana hofu ya chochote kwa sababu anajua kwamba mumewe atamlinda na kumkinga na maudhi.

3. Mume anayehisi kwamba ameshikamana naye na kuridhika naye.

4. Mume anayeshiriki naye katika maongezi matamu yenye hisia tamu. mume anayempa maneno laini, sio maongezi makavu yasiyokuwa na hisia za kimahaba.

5. Anataka mume anayembusu kila anapoagana naye au anapokutana naye. Mke anapenda jambo zuri linalofanywa mara kwa mara hata kama ni dogo, kuliko jambo kubwa linalofanywa kwa kuchelewa au kwa muda mrefu. Busu unalompa kila siku kabla ya kwenda kazini ni bora kwake kuliko “outing” unayompa baada ya miezi sita.

6. Anataka mume anayeyaona yanayofanywa na mkewe kwa ajili yake, hata kama ni madogo. “Attention” ya mume kwa mke ni jambo muhimu mno. Anataka attention yako kwenye mavazi, kwenye chakula na hata mabadiliko madogo anayoyafanya kwenye chumba chenu....sio unakuta kitanda kimebadilishwa mkao unaanza kuponda

7. Mke anataka mume anayemkubali vile alivyo na kuchunga sana usalama wa hisia zake. Usalama wa hisia za mwanamke ni muhimu mno kuliko hata usalama wa uchumi wake. Haitakuwa na maana kama unamnunulia mavazi mazuri, lakini ukawa unaziumiza hisia zake.

8.mke anataka mume mwenye imani asiyetereka wala kuyumbishwa kwa maneno ya dada zake hata wazazi wake anayeweza kujisimamia ,sio kuperekeshwa

Ili kujifunza zaidi namna ya kutunza na kuimarisha mahusiano yako Pia usisahau kusikiliza sauti ya Mungu na kutenga Muda wa kuomba zaidi.