Zimetimia siku tano bila mafaniko ya kupatikana mtoto aliesombwa na Maji Babati



Na John Walter-Babati

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Manyara kwa siku ya tano sasa, bado linaendelea kumtafuta mtoto Salimu Muhazar (12) aliekuwa mwanafunzi wa shule ya Msingi Darajani mjini Babati, aliesombwa na maji wakati wakicheza kando ya mto Muruki January 20 mwaka huu.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Manyara Julishaeli Mfinanga amesema jopo la waokoaji bado linaendelea na zoezi la utafutaji katika maeneo yote yenye vikwazo.

Amesema zoezi hilo lina ugumu ila uwezekano wa kupatikana upo hivyo wanafamilia waendelee kuwa wavumilivu wakati zoezi libaendelea.

Mto huo unatoa maji kutoka ziwa Babati na kupokea maji ya mvua kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Babati ambapo huyasafirisha hadi ziwa Manyara lililopakana na mkoa wa Arusha.

Muungwana Blog inatoa pole kwa wana familia na wakazi wa Babati waliokumbwa na mkasa huo mzito.