Breaking News: Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak afariki dunia


Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak afariki dunia hospitalini jijini Cairo akiwa na miaka 91.

Mubarak alidumu madarakani kwa miongo mitatu kabla ya kung'atuliwa jeshi baada ya maandamano makubwa ya raia.

Alikutwa na hatia ya kula njama katika mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi na kuwekwa kizuizini.

Hata hivyo, hatia hiyo iliondolewa na akaachiwa huru mwezi Machi 2017.

Kifo chake kimethibitishwa na Televisheni ya taifa ya Misri leo Jumanne. Mapema tovuti ya Al-Watan iliripoti kuwa kiongozi huyo alifariki kwenye hospitali moja ya jeshi.

Mubarak alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwezi Januari.

Mtoto wake wa kiume Alaa alisema siku ya Jumamosi kuwa baba yake yupo mahututi.
Endelea kuwa nasi Muungwana blog tutaendelea kukuhabarisha zaidi juu ya habari hii.....