Breaking: Wajumbe wa Jeshi la Zimamoto waliotajwa na JPM sakata lililomng'oa Lugola watinga TAKUKURU na 'Laptop' zao


Waliokuwa Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Makubaliano yaliyosainiwa August 22 2019 kati ya jJeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni ya Rom solution co.ltd wanaodaiwa kupewa laptops na posho za vikao na safari kwa kila kikao USD 800 na kampuni hiyo wameitwa leo TAKUKURU Jijini Dodoma katika mahojiano wakiwa na laptops walizopewa na kampuni hiyo.


Wajumbe hao ni;

Kamishna wa Zimamoto BARAKA S SEMWANZA
Naibu kamishna wa Zimamoto FIKIRI S SALLA
Naibu kamishna wa zimamoto LUSEKELO CHACHULA
Naibu kamishna ULLY O MBURUKO
Mchumi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ….BONIFACE KIPOMELA
Mchumi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji…FELIS MSHANA