https://monetag.com/?ref_id=TTIb Chama cha msalaba mwekundu kimewataka wanchinanchi kujiunga na chama hicho ili kukabiliana na majanga mbalimbali | Muungwana BLOG

Chama cha msalaba mwekundu kimewataka wanchinanchi kujiunga na chama hicho ili kukabiliana na majanga mbalimbali


Na Theo Mwambasi George, Kigoma.

Chama cha Msalaba mwekundu(REDCROSSS) mkoa wa Kigoma kimetoa wito na kuwataka wananchi wa Kigoma kujiunga na chama hicho kwa kufungua matawi katika mkoa huo ikiwa ni moja ya fursa kwa wananchi kutambua na kujua namna gani ya kusaidiana wao kwa wao katika matatizo mbalimbali.

Wito huo umetolewa na mratibu Khalid Seleman pamoja na mratibu msaidizi wake Belias Ngomboka wa chama cha msalaba mwekundu mkoani Kigoma kwa wananchi wa mkoa huo.

Waratibu hao wakizungumza na wananchi jana jioni katika Ngome ya Urusi wamesema kuwa lengo kuu nikutoa semina kwa wananchi hao juu ya chama cha msalaba mwekundu pamoja na kuwafanya watu kujua fursa mbalimbali zinazoweza kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Aidha chama hicho ambacho kimejikita kujitolea katika kutoa huduma za kibinadamu nchini ,kilianzishwa mwaka 1962 kwa sheria ya bunge na.71 ambapo mpaka sasa chama hicho kina wanachama,voluntia na matawi karibu nchi nzima.

Hata hivyo shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama cha msalaba mwekundu ni kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na majanga mbalimbali,kukabiliana na maafa,,kutoa huduma ya kwanza,kutoa huduma kwa wakimbizi mfano waliopo mkoani Kigoma pamoja na kuunganisha familia,ndugu waliopotezana wakati wa majanga ya kijamii.

Sambamba na hilo kuhusiana na suala la Afya chama cha msalaba mwekundu kinahamasisha jamii juu ya mpango wa damu salama,huduma za kujikinga na UKIMWI,huduma za kutunza wagonjwa nyumbani,kushiriki kampeni za afya kwa jamii ikiwemo kuwapeleka watoto kupata chanjo na huduma za upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira kwa ujumla.

Mratibu Khalid Selemani amemalizia kwa kusema kuwa chama cha msalaba mwekundu mkoani kigoma kina miradi mingi ikiwemo mashamba ambayo wananchi wakijiunga na chama hicho itakuwa ni fursa kwao kujikita na kilimo ambacho kitasaidia wanachama kujikwamua kiuchumi huku kujitoa na utu ikiwa ni muhimu katika kusaidia jamii.