Jifunze kuwekeza mambo haya katika Maisha yako

Ili uweze kuwa bora katika maisha yako huna budi kuwekeza mambo mbalimbali ambayo nitayeleza katika makala haya, yatakusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kuwa bora.

Kama ambavyo mara kadhaa nimekuwa nikinukuliwa nikisema ya kwamba hatma ya maisha yako yapo mikononi mwako, hivyo jifunze ni kwa namna gani wewe binafsi utakuwa kiongozi wa maisha hayo, hata mwanafasafa mmoja wa kimataifa Mr Jim Rohn aliwahi kusema ya kwamba huwezi ukasema unataka kutengeneza mwili wako katika misingi ya mazoezi, kisha wewe ukaamua kumuajiri mtu aweze kufanya mazoezi hayo kwa niaba yako, kisha ukategemea mabadiko yaweze kutokea kwako.

 Jim Rohn anasema mabadiliko ya aina hiyo hayapo.

Hivyo kila wakati kama unataka kufanya mazoezi ya mwili ni lazima uweze kufanya wewe mwenyewe, halikadharika katika maisha yako ya kila siku ili uweze kuwa bora ni lazima uweze kufanya vitu wewe mwenyewe ili uweze kuwa bora zaidi, kwa watoto wa mjini wana msemo wao ambao unasema ni vyema ujifunze kupambana na hali yako.

Hii ikiwa na maana ya kwamba ili uweze kuwa bora ni lazima  uwekeze katika mambo yafuatayo;
1. Kusimamia vitu vyako katika ustadi wa hali ya juu pasipo kuambiwa na mtu na pasipo kusimamiwa na mtu mwingine. Watu wengi wanashindwa kufikia kilele cha mafanikio kwa sababu wamekuwa wamekeza muda mwingi katika kufanya kazi bila kuwekeza nguvu na juhudi za kutosha katika jambo hilo.

2. Kila wakati jifunze vitu vipya vitakavyokufanya kuwa bora zaidi. Vitu hivyo vipya ni lazima uviweke katika matendo pia. Wanasema ya kwamba mambo yanabadilika hivyo ni lazima na wewe ujifunze kubadilika ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo. Daima ni lazima ukumbuke hicho unachokijua leo hakitakuwa na thamani baada ya miaka miwili ijayo, hivyo wekeza muda mwingi katika kujifunza vitu vipya.

3. Jifunze kupanga mipango mikakati ya maisha yako.
Maisha bila mipango ni sawa na bure, hivyo kwa kuwa wewe unajua ni nini ambacho unakitaka jitahidi sana kupanga fanya mipango na mikakati itayokusaidia kuwa bora. Yupo mwandishi mmoja jina limenitoka aliwahi sema usipojenga misingi ya maisha yako vizuri yupo mtu utamsaidia kujenga misingi ya  maisha yake.

Hivyo kila wakati ili uweze kuwa bora ni lazima uzingatie hayo ili uweze kuwa bora katika maisha yako.