Kamishna Jenerali wa Magereza akutana na vyombo vya ulinzi na usalama


Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Suleiman Mzee akifanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo alipotembelea leo Makao Makuu ya Jeshi ikiwa ni ziara yake maalum ya kujitambulisha kwa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama tangu aapishwe kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, Februari 3, 2020.

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Seleman Mzee akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Diwani Athumani alipomtembelea ofisini kwake leo mara baada ya  mazungumzo.



 Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akisalimiana na Maafisa wa Uhamiaji alipowasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dar es Salaam leo.