Patrick Aussems ajibu maombi ya Simba kurudi

Aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba Patrick Aussems, amesema kuwa amekuwa akipokea maombi mengi kutoka kwa mashabiki wa Simba wakimtaka arejee kuifundisha klabu hiyo.

Kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii Aussems ameeleza kuwa anaiheshimu Simba na mashabiki wake wote lakini anawatakia kila la kheri na huenda watakutana tena siku nyingine.

'Simba ni klabu kubwa, ina wachezaji wakubwa na mashabiki wa aina yake, nawatakia heri na siku moja pengine tutakutana tena', ameandika.

Aussems alitimuliwa na Simba mwishoni mwa mwaka 2019 na nafasi yake kuchukuliwa na raia mwenzake wa Ubelgiji Sven Vandenbroeck.