https://monetag.com/?ref_id=TTIb Rais Macron azungumzia juu ya sera za Ufaransa kuhusiana na silaha za Nyuklia | Muungwana BLOG

Rais Macron azungumzia juu ya sera za Ufaransa kuhusiana na silaha za Nyuklia

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amearifu kwamba nchi yake inamiliki vichwa vya makombora ya nyuklia visivyozidi 300.

Macron alielezea mikakati ya nchi hiyo kuhusiana na silaha za nyuklia wakati akizungumza katika chuo cha kijeshi mjini Paris.

Macron alisisitiza kwamba anaamini usalama wa Ulaya kwa muda mrefu unategemeana na ushirikiano wenye nguvu baina ya Umoja huo na Marekani. Aliongeza kwamba inapaswa wao kama Ufaransa waongeze uwezo wao wa kujilinda wao wenyewe bila kutegemea mshirika.

Macron pia alisema inapaswa iwepo taasisi ya kimataifa itakayodhibiti suala la kujimilikisha silaha kwa mataifa ya Ulaya.