Samatta dimbani jumapili hii


Kivumbi cha Ligi Kuu ya England kinaendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa, ambapo Wolves watakuwa nyumbani kuwakaribisha Leicester City.

Kocha wa Leicester, -Brendan Rodgers anasema kiungo mkabaji wake Wilfred Ndidi hana uhakika kama atakuwa sehemu ya kikosi chake kutokana na upasuaji wa goti aliofanyiwa katika siku za hivi karibuni huku Ryan Bennett akikosekana kutokana na vipengele vya mkataba wake wa mkopo akitokea Wolves.

Kwa upande wa Wolves, wanaimani mshambuliaji wao mweye nguvu nyingi Adama Traore atakuwa sehemu ya kikosi cha usiku wa leo licha ya maumivu ya bega aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Manchester United, lakini watamkosa Ruben Vinagre anayesumbuliwa na tatizo la misuli.