Taasisi kutoka China yawashika mkono waathirika wa mafuriko Lindi


Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya China inayofanya kazi nchini  (Over Seas Chinese  Services Center) imetoa msaada kwa Wananchi waliopata maafa ya mafuriko mkoani Lindi.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Chama cha Msalaba Mwekwendu Tanzania Red Cross wenye thamani ya sh.milioni 30.Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Taasisi ya China Aston Yi amesema kuwa Tanzania ni China ni familia moja hivyo wanajibu wa kutoa msaada kwa wahanga wa maafa.

Amesema kama Taasisi imeguswa na wahanga wa mafuriko mkoani Lindi hivyo kwani baadhi yao wamepoteza kila kitu hivyo japo wapate vitu hivyo.
Aidha amesema wataendelea kuwa pamoja na watanzania pale panapotokea majanga hayo.

Vitu walivyotolewa kwa wahanga wa mafuriko mkoani Lindi ni Nguo 600  Viatu Jozi 360, Unga Kilogram 2350, Vitabu 1250 pamoja na mashuka  mazito 640.

Nae Meneja wa Kujiandaa na Kukabiliana na Majanga wa Tanzania Red Cross Jonston Weston amesema kuwa Wananchi wa Mkoa wa  Lindi wanahitaji msaada kwani baadhi yao wamepoteza makazi.

Amesema kuwa katika elimu wanayoitoa kwa Wananchi ni pamoja kuwataka kufatilia taarifa za mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuchukua tahadhari mapema.