Timu ya Ruvu Shooting FC yatozwa faini ya Tsh 1,000,000

Mechi namba 232 - Polisi Tanzania FC 3 vs Ruvu Shooting FC 1

Timu ya Ruvu Shooting FC imetozwa faini ya Tsh 1,000,000.00 (milioni moja) kwa kosa la timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi na kusababisha kutokea kwa vurugu zilizoongozwa na mwalimu wa timu hiyo Salum Mayanga pamoja na wachezaji wa timu hiyo,Shabani Kisiga, Emmanuel Martin na Rajabu Zahiri katika mchezo tajwa uliofanyika Februari 22, 2020 uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.

Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni 14(43) ya Ligi Kuu Kuhusu Taratibu za Mchezo.