https://monetag.com/?ref_id=TTIb TRA yakamata bidhaa mbalimbali zilizoingia nchini kwa njia zisizo rasmi | Muungwana BLOG

TRA yakamata bidhaa mbalimbali zilizoingia nchini kwa njia zisizo rasmi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kilimanjaro,imesema haitofumbia macho uingizwaji wa bidhaa za magendo nchini kwa lengo la kulinda mapato ya serikali na usalama wa wananchi baada kukamata bidhaa mbalimbali zilizoingia nchini kwa njia zisizo rasmi,ikiwemo Tani 4.5 za majani ya chai,ambayo yanadaiwa kutumika kutengeneza pombe haramu.

Bidhaa nyingine  zilizokamatwa ni mifuko mbadala iliyochini ya viwangoTani 7,mafuta ya kula lita 9,482,Sukari tani 4.5, Maziwa ya Bruckside lita 186 na vyombo vya usafiri vilivyotumika kusafirisha bidhaa hizo ambavyo ni Magari 8,baiskel 1 na pikipiki 11.

Akizungumza na wanahabari na kutoa taarifa hiyo leo februari 13,2020,Meneja msaidizi wa Forodha mkoa wa Kilimanjaro,Edwin Iwato,amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika kipindi cha mwezi Julai 2019 hadi sasa Februari 2020.

Kwa upande wake Meneja wa mamlaka hiyo ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi,amebainisha thamani ya bidhaa zote zilizokamatwa na kwamba zote zinatoka nchi jirani ya Kenya kwa kupitia njia za zisizorasmi mpakani.