Tshishimbi apigwa faini ya Tsh. 200,000

Mchezaji na nahodha wa timu ya Yanga SC Papi Tshishimbi ametozwa faini ya Tsh. 200,000 (laki mbili) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano (interview) na mdhamini wa Ligi Kuu Azam Media katika mechi iliyofanyika Februari 23, 2020 uwanja wa mkwakwani mkoani Tanga.

Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa kanuni 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.