Watu 31 wameuawa katika shambulizi nchini Mali

Watu 31 wameuawa katika shambulizi  dhidi ya kijiji cha  Odossagou nchini Mali.

Shambulizi dhidi ya kijiji kimoja ambacho kimetajwa kuwa  wakazi wengi ambao ni kabila la Fulani Odossagou nchini Mali limepelekea vifo vya watu 31.

Waziri  mkuu wa Mali kupitia kurasa zake katika mitandoa ya kijamii amesema kwamba idadi ya watu waliofariki katika shambulizi hilo lililoendeshwa dhidi ya kijiji hicho imeongezeka na kufikia watu 31.

Tangazo hilo limefahamisha pia kuwa  operesheni za jeshi  dhidi ya makundi ya wahalifu  zimeanza.

Taarifa zimefahamisha kwamba watu  48 wmefariki wakiwemo wanawake wajawazito  watano katika vijiji tofauti nchini Mali.