Watu 7 wanusurika kifo baada ya kula nyama yenye sumu Handeni

Watu 7 ambao ni walinzi wa maduka yaliopo katikati ya Mji wa Handeni mkoani Tanga wamenusurika kifo baada ya kula mishkaki inayoshukiwa kuwa na sumu waliyopewa na mtu asiyejulikana ambapo mara baada ya kula mishkaki hiyo waliishiwa nguvu na maduka yao kuvunjwa na kuibwa bidhaa mbalimbali pamoja na fedha.

Wakiongea na Channel Ten Baadhi ya majeruhi hao wamesema kuwa siku za hivi karibuni walijiwa na watu wasiojulikana ambapo waliomba kupatiwa eneo la kufanya biashara ya nyama za vipande vidogo maarufu kama mishikaki na walipopatiwa ndipo wakaanza biashara hiyo.

Lakini cha ajabu ni bei ya mishkaki hiyo ilikuwa ni rahisi ikilinganishwa na bei iliyozoeleka mitaani jambo ambalo liliwavutia walinzi hao na usiku wa jana kujikuta wanapewa mishkaki ya bure kwa madai kuwa ilikuwa imebaki kumbe ulikuwa ni mtego wa mhalifu ambapo baada ya walinzi hao kula mishkaki hiyo hali ikabadilika kama wanavyoeleza.

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya mji wa Handeni Dkt. Hudi Shehdadi amethibitisha kuwapokea majeruhi hao.

Godwin Gondwe ni mkuu wa wilaya ya Handeni ambae ameongoza kamati ya ulinzi na usalama hadi kufika hospitali hapo kwa lengo la kuwajulia hali majeruhi hao na hapa akawa na haya ya kusema.

Hata hivyo Channel Ten imeweza kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara ambao maduka yao yamevunjwa na kuibiwa ambapo wamelipongeza jeshi la polisi kwa kufika mapema eneo la tukio.