Wema Sepetu aanza mwaka vizuri, alamba dili la ubalozi wa Rasta


Msanii wa bongo movie Wema Sepetu leo February 21,2020 ametangazwa kuwa Balozi mpya wa Rasta za Angel na kumfanya aanze mwaka vizuri kwa kulamba dili la kwanza toka kuanza mwaka 20202.

Baada ya kupata Ubalozi wa Rasta leo, Wema Sepetu amesema mwaka 2020 umeanza vizuri kwake na yupo imara kuendelea na mapambano.

"Niko strong, wengi wananifuata niwatangazie ila nachozingatia nikitaka kutangaza bidhaa ni ubora wake, sitangazitangazi tu bidhaa, natangaza zile ambazo ni the best kwasababu na mimi pia ni the best"- WEMA