Kwa nini virusi vya corona husambaa haraka miongoni mwa wanadamu

Ni kifurushi kidogo cha nyenzo za jeni iliozungukwa na protini na ukubwa wake ni moja ya elfu ya unywele wa binadamu.

Hata hivyo, virusi hivi hatari kwa jina SARS-CoV-2, tayari vimesambaa katika kila nchi duniani na vimeambukiza zaidi ya nusu milioni ya watu tangu vilipotambulika nchini China mwezi Disemba 2019.

Virusi kama hivi, kutoka familia ya coronavirus pia vinaweza kusababisha maradhi kwa wanyama.

Ni virusi saba vinavyojulikana ikiwemo SARS-CoV-2, ambavyo vimesambaa kutoka kwa wanyama na kuingia kwa binadamu.

Na ndio maana vimehusishwa na milipuko wa magonjwa hatari zaidi katika historia mwaka 1918, 1957, na milipuko ya Influenza pamoja na SARS, MERS na Ebola

Lakini wataalamu wanakubaliana kwamba kirusi hatari kinachosambaa haraka kama hiki cha corona hakijawahi kuonekana.

Hivyo basi tunauliza ni nini haswa kinachofanya virusi vya SARS-CoV-2 kushambulia seli za mwanadamu na kusambaa kwa haraka?

Tafiti kadhaa zinachunguza ni taratibu gani za kibaiolojia virusi hivyo vinatumia ili kuambukiza seli za wanadamu.

Baadhi ya wanasayansi wanaangazia kile kinchoitwa Miba, ambapo miba hiyo yenye umbo la protini hujitokeza katika sakafu yake na kutengeza corona.

Tafiti nyingine zinachunguza njia inayotumika na virusi hivyo ndani ya mwili wa mwanadamu.

Coronavirus ina jina hilo kwa sababu hutokana na protini yenye mwiba inayojitokeza kutoka katika sakafu yake na miba hiyo ndio inayosaidia virusi hivyo kuingia katika seli kulingana na Panagis Galiatsatos, Profesa wa magonjwa ya mapafu na wagonjwa mahututi kutoka chuo kikuu cha tiba cha Johns Hopkins University.

Lengo la virusi hivyo punde vinapoingia mwilini ni kuzaana na ili kufanikiwa kufanya hivyo ni sharti viingie katika seli.

''Virusi vinavyosababishwa na homa ya kawaida, SARS ya 2003 na MERS vyote vina miba , na kile kinachobaini jinsi vitakavyoingia katika seli ni aina ya receptor itakayotumika'' , anaelezea mtaalam.

Baadhi ya wanafunzi wamefanikiwa kuonyesha kwamba SARS-CoV-2 hujiondoa katika receptor - ama protini kwa jina ACE2 .

Protini hii hupatikana katika maeneo mengi ya mwili wa mwanadamu kama vile mapafu, moyo, figo na matumbo na kazi yake kuu ni kupunguza shinikizo la damu.

"ACE2 ipo katika sakafu ya seli na wakati virusi hivyo vinapoitambua, vinashikana na hivyobasi kuingia katika seli , kulingana na Sarah Gilbert, profesa wa chanjo katika chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza .

Punde tu vinapoingia ndani , vinatumia seli hiyo kama kiwanda cha kuzalisha virus zaidi .

Baadaye kinatoroka katika seli ambapo kinawacha ganda moja la kirusi kinachoendelea kuambukiza seli nyengine.

Virusi vya mapafu , kama vile mafua , hupenda sana kuzaana puani na kwenye koo ambapo vinaweza kusambazwa rahisi kupitia kikohozi na kupiga chafya.

Lakini kuna virusi vingine ambavyo huzaana katika eneo la chini la mapafu , ambapo husambaa kwa urahisi lakini huwa hatari zaidi.

Kipengele muhimu
SARS-CoV-2, hatahivyo vina tabia tofauti. Hupatikana katika mapafu ya juu na yale ya chini , vikisambaa kupitia kikohozi na mapafu ya chini na kusababisha magonjwa ya mapafu ambayo yanaweza kuwa hatari zaidi.

ACE2 ni nyingi mwilini na hupatikana katika viungo vingi vya mwili wa mwanadamu, kulingana na profesa Galiatsatos.

Ni katika seli za mdomo, koo, figo moyo na hata utumbo ambapo baadhi ya wagonjwa huhisi kisunzi na kuharisha.

Lakini cha kutishia ni kwamba virusi hivi pia viko katika alveoli sehemu nyepesi za hewa kwenye mapafu ambapo uhamishaji wa gesi hufanyika. "

Wakati virusi hivyo vinapoharibu seli kulingana na mtaalamu huyo kunakuwepo baadhi ya dalili zinazopatikana katika mtu aliyeambukizwa na covid-19 kama vile tatizo la kupumua, kikohozi ambacho hutokea wakati mapafu yanajaribu kukabiliana na maambukizi.

Dalili na maambukizi
Mojawapo ya tofauti kati ya SARS-CoV-2 na viruis vya corona kama vile SARS ya 2003 ama MERS , ni kwamba virusi hivi huzaana kwa haraka.

Hatua hiyo husababisha dalili za ugonjwa huo kuonekana haraka na kwamba mgonjwa anaweza kujitenga kwa haraka bila kusababisha maambulkizi zaidi.

Katika virusi vya covid 19 , dalili hazionekani haraka na watu wanaweza kupata maambukizi yake na kuusambaza bila kuonyesha dalili za ugonjwa huo.

"SARS (2003) vilikuwa virusi vilivyozaana katika mapafu na kuambukizwa kwa urahisi kwa sababu dalili zake zilionekana kwa haraka na mgonjwa aliweza kujitenga kwa haraka kulingana na profesa David Hymann, mtaalamu wa magonjwa ya maambukizi ambaye aliongoza ujumbe wa WHO wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo.

Lakini virusi vyote vyote viko tofauti , na virusi hivi vipya vinaonekana kuwa na uwezo wa kusambaa kwa haraka na kwa urahisi miongoni mwa bindamu.

''Tunaamini kwamba mtu anaweza kuanza kumuambukiza mtu mwengine kabla ya dalili kuonekana , siku moja kabla , na baadaye kuendelea kuambukiza kwa takriban siku saba'', anaongezea.

Hapa ndiposa hatari kubwa ya SARS -CoV-2 huonekana na hivyobasi ndio sababu serikali nyingi zinasisitiza kuhusu kukaa mbali. Virusi hivyo vinaweza kuishi iwapo vitapata mtu mwengine wa kuambukiza .

Wakati mtu anaposalia nyumbani kwa siku 14 inapunguza fursa ya kuambukiza mtu mwengine.

''Kwa sasa hiyo ndio njia pekee inayoweza kutumika . Juhudi zinafanywa kutafuta chanjo ama tiba , lakini hatua zilizopigwa kisayansi sio za haraka kama vile tunavyohitaji na kila kitu kitachukua muda'', alisema Panagis Galiatsatos.

Katika kitabu cha Art of War "Sun Tzu anasema kwa wewe kuweza kushinda vita ni sharti umjue adui yako . lakini unapotambua kwamba adui yako ni mjanja unalazimika kuwa mvumilivu . Ni hicho ndicho naweza kusema kuhusu virusi hivi.

Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 31 Machi 2020
Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.