Serikali haina mpango wa kuwaongezea muda wakandarasi


Serikali imesema haina mpango kwa sasa wa  kuwaongezea muda makandarasi wa miradi ya umwagiliji na ujenzi wa maghala unaofanyika katika mkoa wa Morogoro chini ya maradi wa kuongeza uwezo wa uzalishaji na tija katika zao la mpunga(ERPP)

Akiongea mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu katika miradi kumi na moja (11) iliyopo mkoani hapo  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Gerald Kusaya amesema wakandarasi hao walipewa kazi tangia tarehe 15 Aprili, 2015  ambapo mpaka sasa ipo miradi ambayo haijakamilika.

Awali bwana Benjamini Kiaruzi mhandisi Skimu ya umwagiliaji ya Kigugu  kutoka Gopa Contractors (T) Ltd ameomba serikali kumpa muda wa nyongeza kutokana na changamoto za uwepo wa mvua  nyingi na kucheleweshewa fedha za mapipo ya kwanza nay a pili.

Akijibu maombi ya mhandisi  huyo Bw. Kusaya amesema ifikapo tarehe 30 April 2020 serikali itahitaji kupokea miradi yake yote ikiwa tayari na kwa miradi ambazo hazijawa tayari serikali itachukua hatua kulingana na mkataba husika.

“Mimi sitaki kusikia changamoto nataka kuona wakulima wanakabidhiwa miradi, ni vizuri kufahamu kwamba wakulima wanateseka kwa kusubiri miradi hii ikamilike ili waanze kulima yapo mazao yanakuka shambani wanashindwa kumwagilia kwa sababu yenu kwa kweli hatutavumilia ikifaika mwisho wa April” alisema Gerald Kusaya.

Aidha miradi hiyo inaghamu Dola za kimarekani Milioni 16.5 ambapo malengo yake ni Kupeleka mbegu mpya za mpunga kwa wakulima ,Kukarabati na kuboresha miundombinu ya Skimu Tano(5) za umwagiliaji za Mvumi, Kilangali Seed Farm-ASA, Msolwa Ujamaa, Njage na Kigugu irrigation scheme) ili kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya Maji yenye ufanisi katika kilimo cha umwagialiaji

Hata hivyo mradiulilenga  Kujenga maghala matano(5) katika maeneo ambako skimu za umwagiliaji zimeboreshwa kwa lengo la kuhifadhi kabla ya kupatikana soko lenye tija Zaidi alisema Bwana Kusaya.

Hata hivyo amewataka wakulima watakaofaidika na miradi hiyo ikiwemo maghala kushiriki katika ulinzi wa miradi yao ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kutafuta njia mbadala ya kuendeleza za namna ya kukarabati miundombinu hiyo kwa kutoa asilimia katika mauzo ya mazao yao.

Ili kuhahikisha  usimamizi wa miradi hii unatekelezwa kwa ufasaha Katibu mkuu ameitaka tume ya umwagiliaji  kuhakikisha wanampatia taarifa za kila baada ya siku tatu na kuahidi kwamba atazifanyia kazi mara tu  azipatapo.