Uhispania tishio yaipiku China, Italia vifo vya virusi vya corona


Idadi ya vifo nchini Uhispania kutokana na virusi vya corona imepanda kwa zaidi ya watu 700 leo, na kuipiku China na sasa ni nchi ya pili baada ya Italia kwa kurekodi idadi kubwa ya vifo, wakati janga hilo likisambaa kwa kasi barani Ulaya.

Uhispania imerekodi vifo vya watu 738 vilivyotokea leo, na kufikisha jumla ya 3, 434 ikiwa ni zaidi ya China ambayo in vifo 3,285.

Fernando Simón, ni mkurugenzi wa kituo cha uratibu wa majanga ya dharura katika wizara ya Afya nchini UhispaniaNchini India, taifa kubwa kabisa duniani, serikali imewafungia majumbani raia wake bilioni 1.3, wakati nchini Marekani, wabunge wameidhinisha mpango mkubwa wa msaada wa ndani wa trilioni 2.

Nchini Uingereza, Mwanamfalme Charles ambaye ana umri wa miaka 71, ameambukizwa virusi hivyo. Italia ndilo taifa lililoathirika zaidi Ulaya, likiwa na zaidi ya maambukizi 69,000 na vifo 6,800.

Bunge la Ujerumani limeidhinisha hatua za kuiwezesha serikali kutoa msaada wa zaidi ya euro trilioni moja kuwasaidia raia wake milioni 83.