Zaidi ya wafungwa 4,000 waachiwa huru Ethiopia ili kudhibiti corona


Zaidi ya wafungwa 4,000 wameachiwa huru nchini Ethiopia ikiwa ni hatua ambayo serikali hiyo imechukua ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Mwanasheria Mkuu alisema siku ya Jumatano kuwa wafungwa wote walioadhibiwa kwa kesi ndogondogo na wanawake ambao wana watoto ndio wataoachiwa huru.

Wageni ambao walishtakiwa kwa makosa ya usafirishaji haramu na dawa za kulevya wataachiwa huru pia na kurudishwa katika nchi zao .

Mhariri wa jarida ambaye alirejea nchini Ethiopia mara baada ya Waziri Mkuu Ahmed Abiy kuingia madarakani mwaka 2018 wakati ambao maelfu ya wanasiasa waliachiwa huru na hali ya taifa kuwa kwenye dharura kusitishwa huku vyama vya kisiasa vikivunjwa.

Lakini mwandishi huyo alibaki na mashtaka ya kukwepa kodi hivyo kuadhibiwa kifungo cha miaka saba tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Abiria wote wanaowasili Ethiopia kukaa karantini katika hoteli
Hatua nyingine ambazo Ethiopia imezichukua kukabiliana na maambukizi ya corona ni wafanyakazi wengi kufanyia kazi nyumbani pamoja na kufunga mipaka yake yote.

Abiria wote wanaowasili Ethiopia wanapaswa kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hoteli ambazo zimechaguliwa na mamlaka.

Raia wa Ethiopia ambao watashindwa kulipia gharama za karantini, serikali gharamia.

Zaidi ya wasafiri 400 wameanza kukaa katika karantini kwa lazima, kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini humo.

Taifa hilo limefunga kumbi zote za starehe za usiku.

Mpaka sasa Ethiopia ina wagonjwa 12 wa Covid-19.