Fahamu kuhusu tatizo la hangover na suluhisho lake

Kuna pombe au vilevi vya aina tofauti kama vile bia, wine, pombe kali. Watu wengi hupenda kujiburudisha kwa kunywa vinywaji hivi na kati yao kuna ambao wanajikuta baada ya kunywa kwa kupitiliza wamepata hali ya kutapika, kichwa kuuma, kizunguzungu, usingizi mkali, uchovu wa mwili n.k, hali ambayo ni maarufu kama “Hangover”.

Hali hii inaweza kuanza masaa machache baada ya kuacha kunywa kilevi hadi masaa 24. Kikubwa kinachosababisha hali hii ni kuwa na kiasi kikubwa kupitiliza cha kilevi mwilini. Hii inatokana na kwamba kiasi cha kilevi kinacho tolewa mwilini hakibaliki kadiri ya kiasi cha kilevi ambacho mtu atatumia (Zero order kinetics).

Inamaana kama litre 1 moja ya kilevi inatolewa ndani ya saa moja, kwahivyo endapo mtu atakunywa litre 5 za kilevi ndani ya saa moja bado kiasi ambacho kitatolewa mwilini kitabaki kuwa litre moja ndani ya saa moja. Hali hii inasababisha ulimbikaji wa pombe mwilini. Ulimbikaji huu huongeza kasi katika athari za pombe mwilini. Hali ambayo inafahamika kama “hangover”

Uwezo wa mwili kukabiliana na kiasi cha kilevi ambacho mtu amekunywa inatofautiana kati ya mtu hadi mtu kulingana na:

Kiasi cha pombe ambacho mtu anakunywa mara kwa mara.  Endapo mtu hunywa pombe mara kwa mara, uwezo wa mwili wake kukabiliana na pombe huongezeka.
Vinasaba vya mtu ambavyo vinaamua kiasi na aina za protini za umeng’enyuaji zinazotengenezwa.
Magonjwa ambayo yaweza sababisha kupungua au kuongezeka kwa kiasi cha uondoaji wa pombe.
Utumiaji wa pombe na dawa ambazo zinaathiri mlorongo wa  umeng’enyuaji wa pombe.

Je, ninawezaje kuondoa hali ya “Hangover”?
Hali hii ya hangover huisha pale ambapo mwili umeweza kutoa pombe kufikia kiasi kidogo hivyo mwili unahitaji muda kuendelea kuondoa pombe ili uweze kurejea hali ya kawaida. Katika muda huu unaweza kufanya yafuatayo ili kuusaidia mwili kuondoa pombe hii:

1. Kunywa maji ya kutosha.
2. Kula chakula chenye vitamin B complex vinavyohitajika katoka umeng’enyuaji wa pombe kama vile nyama aina nyingi( ng’ombe, mbuzi, kuku, samaki), mayai, maziwa, viazi, maharagwe n.k
3. Kula /kunywa vitu vyenye sukari