Trump awataka Wamarekani wavumilie wiki mbili za maumivu


Marekani leo imeripoti vifo 4087 na wagonjwa wa corona 189,800, Rais Trump amewataka Wamarekani kuvumilia na kujiandaa na kipindi hiki kigumu cha wiki mbili zenye maumivu makubwa huku akisema Serikali yake inapambana na anaamini maambukizi yatapungua.